1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Korea Kusini yataka Korea Kaksazini idhibitiwe

Amina Mjahid
3 Juni 2023

Waziri wa ulinzi wa Korea Kusini Lee Jong-sup amesema baadhi ya Mataifa ulimwenguni yanafumbia macho tabia isiyokubalika ya Korea Kaskazini

https://p.dw.com/p/4S9co
Gemeinsame Militärübung der USA und Südkorea
Picha: Defense Ministry/ZUMAPRESS/picture alliance

Amesema tabia hiyo inahatarisha na kudhoofisha vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya mipango ya makombora na silaha za nyuklia ya Korea Kaskazini. 

China na Urusi zilipuuzia wito wa Marekani kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuikosoa Korea Kaskazini kwa jaribio lake la hivi karibuni, la kurusha satelaiti na badala yake kuilaumu Marekani kuwa inaongeza mvutano katika rasi ya Korea. 

Lee Jong-sup amesisitiza umuhimu wa ushirikiano wa usalama kati ya taifa lake, Marekani na Japan ili kuikabili Korea Kaskazini.