1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kongo yatumaini kupata suluhisho ya mchuano dhidi ya Chile

3 Juni 2026

Timu ya taifa ya kandanda ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inatumai kupata suluhisho baada ya mechi yao ya mwisho kuelekea kombe la dunia la FIFA, dhidi ya Chile kufutwa na mamlaka za Uhispania.

https://p.dw.com/p/5Enuu
Mechi ya kirafiki 2019 | DR Kongo na  Algerien | Paul-Jose M’Poku (kushoto) na Ismael Bennacer (kulia)
Mechi ya kirafiki kati ya Kongo na Algeria mnamo 10.10.2019 katika uwanja wa Mustapha Tchaker Picha: Ryad Kramdi/AFP

Timu hiyo ya Kongo ilikuwa imepangwa kucheza dhidi ya Chile tarehe 9 Juni katika mji wa La Línea de la Concepción, lakini meya wa eneo hilo Juan Franco alizuia mechi hiyo kufanyika kutokana na wasiwasi wa kiafya.

Franco ameiambia redio Cope ya Uhispania kwamba wataalamu wa eneo hilo na wale wa jimbo la Andalusia walisema nyaraka zilizowasilishwa na ujumbe wa Congo  zilionekana kutoridhisha na wakachagua ''njia ya tahadhari ya kiwango cha juu zaidi.”

Shirikisho la Soka la Congo (FA) limesema kuwa hatua zote muhimu zilichukuliwa ili kutimiza masharti yote ya kiafya na kimichezo, na kwamba "linazingatia kikamilifu taratibu za kimataifa.”