1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kongo yafungwa 2-1 na Chile mchezo kuelekea Kombe la Dunia

10 Juni 2026

Timu ya taifa ya kandanda ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo imepoteza mechi yake yake ya mwisho ya maandalizi kabla ya kuanza michuano ya Kombe la Dunia kwa kukubali kichapo cha bao 2-1 walipokutana na Chile.

https://p.dw.com/p/5F6g5
Ubelgiji 2026 | Mchezaji wa timu ya taifa ya kandanda ya DR Congo, Cedric Bakambu akiwa mazoezini.
Mchezaji wa timu ya taifa ya kandanda ya DR Congo, Cedric Bakambu akiwa mazoezini.Picha: Nicolas Economou/REUTERS

Timu hiyo, The Leopards, ambayo maandalizi yake kuelekea Kombe la Dunia yaliingia kiwingu kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola nchini Kongo, ilicheza mechi hiyo bila kuwepo mashabiki kwenye mji wa Orleans nchini Ufaransa.

Hapo kabla mechi hiyo ilikuwa ichezwe kusini mwa Uhispania, lakini meya wa mji mchezo huo ulikopangwa alikataa kutoa kibali kwa wasiwasi wa virusi vya Ebola licha ya kikosi cha Kongo kupiga kambi barani Ulaya hata kabla ya mlipuko wa sasa.

Kongo inarejea kucheza Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1974 na imepangwa kundi K ikiwa pamoja na Ureno,  Colombia na Uzbekistan.