Kongamano la Kimataifa la Vyombo vya Habari | Masuala ya Jamii | DW | 28.06.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Masuala ya Jamii

Kongamano la Kimataifa la Vyombo vya Habari

Kongamano hilo la nane lililoanza Jumatatu tarehe 22 hadi Jumatano tarehe 24 Juni mjini Bonn, liliwaleta pamoja wajumbe takriban 2,000 kutoka mataifa mbalimbali kote duniani, wengi wao wakiwa waandishi wa habari.

Miongoni mwa mada zilizojadiliwa ni usalama wa mitandao ya kijamii, sera za kigeni katika kuripoti mizozo ya kimataifa, matumizi ya mtandao wa mawasiliano wa intaneti barani Afrika na njia za kuulinda uhuru wa vyombo vya habari.

Unagana na Josephat Charo katika kipindi cha Maoni Mbele ya Meza ya Duara akiwa pamoja na Michael Andindilile, Mkuu wa Shule kuu ya Waandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma, Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania. Simaloi Dajom Otieno, Naibu Mkurugenzi wa Vipindi, kampuni ya Royal Media Services, inayomiliki Redio Citizen, na Faustine Peter Nyanda, Mkuu na Muasisi wa asasi ya kimataifa inayojihusisha na masuala ya ulinzi na usalama Afrika na masuala ya uhamiaji, International Campaign for Africa, mjini Zurich Uswisi.

Kusikiliza maoni haya bonyeza alama ya spika hapo chini.

Mwandishi:Josephat Charo

Mhariri:Mohammed Abdulrahman

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com