1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kaskazini

Kim aongoza gwaride la kijeshi

Lilian Mtono
14 Machi 2024

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un siku ya Jumatano aliongoza gwaride la kijeshi lililohusisha vikosi vya vifaru, shirika la habari la nchini humo KNCA limearifu.

https://p.dw.com/p/4dUPC
Korea Kaskazini yajaribu kombora | Kim Jong-un
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un akiwa na baadhi ya maafisa wa kijeshi walipokwenda kushuhudia jaribio la ufyatuaji wa kombora kutokea baharini, Januari 28, 2024Picha: KCNA via REUTERS

Kulingana na KNCA, Kim pia alieleza kuridhishwa na namna aina mpya ya kifaru cha kivita kilivyofanikiwa kwa mara ya kwanza kuonyesha uwezo wake wa kushambulia, katika kile ambacho KNCA imekiita gwaride la mafunzo.

Shughuli hiyo ya kijeshi iliandaliwa maalumu kwa ajili ya kukagua uwezo wa kupambana wa vikosi vya vifaru na kuviwezesha kuelewa mbinu za kushambulia katika operesheni tofauti tofauti.

Mafunzo hayo ya vifaru yanachukuliwa kama jibu la siku 11 za luteka za kila mwaka za kijeshi kati ya Korea Kusini na Marekani zinazotarajiwa kumalizika siku ya Alhamisi. Taifa hilo linaona mazoezi ya wapinzani wake kama maandalizi ya uvamizi.