Kiasi watu 350,000 wamehamishwa kutokana na mafuriko | Matukio ya Kisiasa | DW | 26.08.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Kiasi watu 350,000 wamehamishwa kutokana na mafuriko

Mto Indus katika eneo la kusini ya jimbo la Sindh nchini Pakistan umezamisha vijiji vingine kadha leo, na maafisa wameamuru watu zaidi ya lakini tatu kuhama katika maeneo yao.

default

Watu walionusurika na mafuriko nchini Pakistan wakipokea misaada kutoka kwa mashirika ya kutoa misaada.

Mto  Indus  katika  eneo  la  kusini  ya  jimbo  la  Sindh nchini  Pakistan  umezamisha  vijiji  vingine   kadha  leo , na  maafisa  wameamuru  watu   zaidi  ya   350,000 kuhamishwa.

Kiasi  cha  watu  laki  tatu  hadi  laki  tatu  na  nusu wataathirika   katika  eneo  la  Thatta, ambalo  ni  wilaya inayoishi  karibu  watu  laki  nane, amesema  Kher Mohammad  Kaloro, mkurugenzi  wa   mamlaka  ya operesheni  za  uokozi  katika  jimbo  lililokumbwa  na maafa  la  Sindh.

Mafuriko  yamevunja  matuta   mamwili,  ya  kuzuwia  maji na  kuilazimu  serikali  kuwaomba  watu  kuondoka  kutoka katika  eneo  hilo  la  Sajawal, mtu  mdogo  unaoishi  watu wapatao  28,000. Maji  pia  yanaelekea   katika   miji  ya Qambar  na  Shadadkor  na  watu  wengi  zaidi wataathirika  ameongeza  Kaloro.

Mara  baada  ya  tangazo  hilo  kutolewa  kwa  njia  ya vipaza  sauti  katika  misikiti  mjini  Sajawal,  biashara zilifungwa  na  watu  walianza   kufunga   chochote walichonacho  ambacho  wanaweza  kukichukua.

Mamia  ya  watu  wamekimbia  mji  huo  kwa  magari, malori na   mikokoteni  ya  ng'ombe. Jeshi  hata  hivyo  lilikuwapo kuwaokoa  watu  ambao  huenda   wakaachwa . Meja jenerali  Shaukat Iqbal , kamanda  wa  jeshi  katika  eneo hilo, amesema  kuwa  maboti  ya  jeshi  la  majini yatatumika  na  helikopta  mbili   zinaangalia  hatua  hizo za  uokozi.

Mafuriko  yaliyosababishwa  na  mvua  kubwa  za  masika mwezi  mmoja  uliopita  yameathiri   zaidi  ya  watu  milioni 17.2, ikiwa  ni  pamoja  na  watu  milioni  3.8  katika  jimbo la  Sindh, na  kusababisha  vifo  vya   zaidi  ya  watu  1,500 kwa  mujibu  wa  mamlaka  ya  kushughulikia  maafa nchini  Pakistan.

Daniele Donati  wa  shirika  la  kilimo  na  chakula  la umoja  wa  mataifa  FAO  amesema  kuwa  hekta  milioni 3.2  za   mazao  zimeharibiwa  na  mafuriko  na  kwamba ng'ombe  wapatao  200,000  wameuwawa  katika  jimbo  la Sindh  na  Khyber-Pakhtunkhwa  pekee.

Wafanyakazi  wa  kutoa  misaada   wamekuwa wakihangaika   kuwafikia  watu  waliotawanyika  ambao wanaishi  hivi  sasa  katika  kambi   za  kutolea  misaada, ama  wako  katika  maeneo  ya  wazi  wakiwa  hawana chakula , dawa  ama  maji  safi  ya  kunywa.

Umoja  wa  mataifa  umesema  wiki  hii   kuwa  kiasi   watu 800,000  bado  wamekwama   ambapo  hawana mawasiliano   na  sehemu  nyingine  za  nchi  hiyo, na zinahitajika  helipokta  zaidi   kuwapelekea   vyakula.

Waziri  wa   kilimo  cha  umwagiliaji  katika  jimbo  la  Sindh amesema   kuwa  maji  yamekuwa  yakileta  mbinyo  dhidi ya  matuta  ya  kuzuwia  maji  katika  vijiji  vya  Garni Khuda Bakhsh, ambako  waziri  mkuu  wa  zamani  wa  Pakistan Benazir  Bhuto  na  baba  yake, pamoja  na  kaka  zake wawili  wamezikwa.

Katika  eneo  karibu  na  bahari  ya  Arabia , maafisa wanahofu  kuwa   wilaya  ziliziko  katika  maeneo  ya  pwani huenda  zikakumbwa  na  mafuriko  katika  siku  zijazo, kutokana  na  mafuriko  kusogea  upande  wa  kusini pamoja  na  dhoruba  baharini.

Katika  harakati  za  uokozi , shirika  la  kimataifa  la wahamiaji IOM  limesema   kuwa   watu  milioni  4.5  bado wanahitaji  sehemu  za  kuishi  kwa  dharura.Mjini Washington  ambako  serikali  ya  Marekani  imeiweka Pakistan  katika  mstari  wa  mbele  katika  juhudi  za kupambana  na  kundi  la  Taliban  nchini  Afghanistan , afisa  wa  Marekani  amesema   kuwa  Taliban  wanapanga kuwashambulia  wafanyakazi  wa  kigeni  wa  kutoa misaada   ambao  wako  katika  kazi  ya  kusambaza misaada.

Mwandishi: Sekione  Kitojo / AFPE / DPAE

Mhariri:

 • Tarehe 26.08.2010
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/OxFc
 • Tarehe 26.08.2010
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/OxFc
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com