1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiHaiti

Kenya yasimamisha mpango wa askari wake kwenda Haiti

Sudi Mnette
13 Machi 2024

Kenya imeamua kusitisha mipango ya kutuma polisi kwa taifa la Haiti lililokumbwa na ghasia chini ya mpango wa kimataifa unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.

https://p.dw.com/p/4dRqS
Watu wa Haiti wanakimbia huko Port-au-Prince
Watu wanatembea na mali zao wakikimbia vurugu karibu na nyumba zao, huko Port-au-Prince, Haiti Machi 9, 2024Picha: Ralph Tedy Erol/REUTERS

Hatua hiyo imekuja baada ya Waziri Mkuu wa Haiti Ariel Henry kukubali kujiuzulu huku magenge yenye silaha yakidhibiti sehemu kubwa ya taifa hilo la Caribbean.

Katibu katika wizara ya mambo ya kigeni ya Kenya Korir Sing'oei amenukuliwa na AFP akisema "Kumekuwa na mabadiliko ya makubwa ya hali kutokana na kutokuwepo kwa utawala wa sheria na kujiuzulu kwa Waziri Mkuu wa Haiti."

Hata hivyo Sing'oei amesema Kenya imesalia kujitolea "kutoa uongozi kwa MSS," akimaanisha ujumbe wa Msaada wa Usalama wa Kimataifa ambao uliidhinishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Oktoba mwaka jana.