1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaHaiti

Kenya yajizuia kupeleka askari nchini Haiti

Sudi Mnette
13 Machi 2024

Kenya imeuzuia mpango wake wa kupeleka askari 1,000 mchini Haiti kufuatia kongezeka kwa ghasia kubwa katika taifa hilo la Carebbean huku Waziri Mkuu, Ariel Henry akiwa ametangaza kujiuzulu.

https://p.dw.com/p/4dSDG
Haiti Port-au-Prince | vurugu za magenge ya kihalifu
Askari wa Kitengo cha ulinzi wa Ikulu ya Kitaifa wakiwa katika ulinzi wa kuzunguka moja ya vituo vitatu vya katikati mwa jiji baada ya kupambana na shambulio la magenge huko Port-au-Prince, Haiti,Machi 9. 2024.Picha: Odelyn Joseph/AP/picture alliance

Taarifa kutoka serikalini nchini Kenya zinasema hatua hiyo ni baada ya kuongezea kwa ghasia ambazo zinashika kasi zaidi, ikiwa pia ni baada ya tangazo la kutaka kujiuzulu kwa Waziri Mkuu, Ariel Henrybaada ya kuundwa baraza la urais.

Katibu katika wizara ya mambo ya kigeni ya Kenya Korir Sing'oei amenukuliwa na Shirika la Habari la Ufaransa AFP akisema "Kumekuwa na mabadiliko ya makubwa ya hali kutokana na kutokuwepo kwa utawala wa sheria na kujiuzulu kwa Waziri Mkuu wa Haiti."

Msimamo wa Kenya katika jitihada za amani za Haiti

Hata hivyo Sing'oei amesema Kenya imesalia katika juhudi za kujitolea "kutoa uongozi kwa MSS," akimaanisha mpango wa Msaada wa Usalama wa Kimataifa ambao uliidhinishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Oktoba mwaka jana.

Waziri Mkuu wa Haiti Ariel Henry
Waziri Mkuu wa Haiti Ariel Henry akitoa muhadhara katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Marekani (USIU) mjini Nairobi, Kenya, Ijumaa Machi. 1, 2024.Picha: Andrew Kasuku/AP Photo/picture alliance

Zaidi aliongeza kwa ufafanuzi "Bila ya utawala wa kisiasa nchini Haiti, hakuna utulivu ambao utakaokiwezesha kikosi cha polisi kuwajibika, hivyo serikali itasubiri kuanzishwa kwa mamlaka mpya ya kikatiba nchini Haiti, kabla ya kuchukua maamuzi zaidi kuhusu suala hilo."

Kauli ya Marekani baada ya uamuzi wa Kenya

Kujibu tangazo la Kenya, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Matthew Miller aliwaambia waandishi wa habari, "Nitakuwa na wasiwasi bila shaka kuhusu ucheleweshaji wowote, lakini hatufikirii kwamba kama kuna uhitaji wa kucheleweshwa."

Mwezi Oktoba Kenya ilikubali kuongoza timu ya polisi ya kimataifa iliyoidhinishwa na Umoja wa Mataifa nchini Haiti, lakini mahakama kuu ya nchi hiyo ilichagiza zoezi hilo mwezi Januari kwa kutoa uamuzi kwamba lilikuwa kinyume na katiba, kwa kile kilichoelezwa kutokuwepo kwa makubaliano juu ya upelekaji wa aina hiyo ya askari baina ya nchi hizo mbili.

Soma zaidi:Kenya bado yatafakari kupeleka askari nchini Haiti

Katika utetezi wake Rais wa Kenya William Ruto alisema kuwa yeye na Waziri Mkuu Henry wameshuhudia kutiwa saini kwa mikataba ya maelewano kati ya Kenya na Haiti Machi Mosi, kusafisha njia ya kupelekwa kwa kikosi hicho.

Katika majuma ya hivi karibuni, mzozo wa Haiti umekua mkali zaidi hali iliyoambatana na  kuonekana kwa miili ya watu iliyozagaa barabarani, magenge ya watu wenye kujihami kwa silaha wakiharibu miundombinu hali ambayo ikigubikwa na mashaka ya kuongezeka kwa njaa.

Chanzo: AFP