1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiKenya

Kenya kupatiwa mkopo wa dola milioni 976 na IMF

11 Juni 2024

Kenya imefikia makubaliano ya mwanzo ya kufungua njia ya kupatiwa mkopo wa dola milioni 976 na shirika la Fedha la Kimataifa,IMF.

https://p.dw.com/p/4gthE
Mkuu wa Shirika la Fedha Ulimwenguni IMF Kristalina Georgieva
Mkuu wa Shirika la Fedha Ulimwenguni IMF Kristalina GeorgievaPicha: Fayez Nureldine/AFP

Katika tamko lake bodi hiyo imesema fungu la kwanza la dola milioni 120 litatolewa mara tu baada ya kuhakiki uwezo wa Kenya wa kulipa madeni.

Licha ya kukabiliwa na changamoto za kifedha tangu mwaka 2022 Kenya imeweza kuuza hati fungani,thamani ya Euro bilioni 1.5 kwenye masoko ya kimataifa.

Hatua hiyo imeondoa wasiwasi juu ya nchi hiyo kushindwa kulipa madeni yake na pia imerejesha imani miongoni mwa wawekezaji vitega uchumi.