1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela Merz afanya ziara ya kwanza ya Ghuba

Josephat Charo
5 Februari 2026

Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz ameanza ziara yake ya kwanza ya eneo la Ghuba itakayompeleka Saudi Arabia, Qatar na Umoja wa Falme za Kiarabu.

https://p.dw.com/p/5869K
Kansela Merz alipokelewa kwa heshima za kijeshi alipowasili mjini Riyadh 04.02.2026
Kansela Merz alipokelewa kwa heshima za kijeshi alipowasili mjini Riyadh 04.02.2026Picha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance

Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz yuko mjini Riyadh, Saudi Arabia, kituo cha kwanza cha ziara yake ya kwanza katika eneo la Ghuba, itakayompeleka pia Qatar na Umoja wa Falme za Kiarabu. Merz ilipokelewa kwa heshima za kijeshi alipowasili Riyadh jana jioni.

Merz alisema Ujerumani inatafuta ushirikiano wa karibu zaidi katika eneo la Ghuba ili kulinda nafasi yake katika mpangilio wa kimataifa unaobadilika haraka, kabla kuanza safari ya kwenda Saudi Arabia, Qatar na Falme za Kiarabu.

Merz alisema Ujerumani ilitaka kutanua mazungumzo ya kimkakati na mataifa hayo matatu katika eneo hilo tajiri na muhimu kimkakati ili kuimarisha usalama wa muda mrefu, uhusiano wa kiuchumi na minyororo ya usambazaji, ikiwa ni pamoja na mafuta na gesi.