Jeshi la Nigeria lauwa wapiganaji 26 wa Boko Haram | Matukio ya Afrika | DW | 26.02.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Afrika

Jeshi la Nigeria lauwa wapiganaji 26 wa Boko Haram

Wapiganaji wasiopungua 26 wa kundi la kigaidi la Boko Haram wameuawa, baada ya kuivamia kambi ya watu waliopoteza makaazi yao kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Kikosi Maalum cha Kupambana na Ugaidi cha Jeshi la Nigeria.

Kikosi Maalum cha Kupambana na Ugaidi cha Jeshi la Nigeria.

Jeshi la Nigeria linasema kuwa shambulizi hilo la jana (Feb. 25) katika mji wa Dikwa jimbo la Borno, pia lilisababisha vifo cha mwanajeshi mmoja na mwanamgambo mmoja wa kundi la ulinzi la kiraia.

Taarifa ya jeshi hilo inasema wakaazi wanne wa kambi hiyo, wanajeshi watatu na waasi kadhaa walijeruhiwa, wengi wao wakiwa na hali mbaya.

Kundi la Boko Haram, ambalo linataka kuanzisha utawala unaofuata tafsri yake ya Uislamu, limeshahusika na vifo vya maelfu ya watu kaskazini mashariki ma Nigeria, Cameroon, Niger na Chad tangu mwaka 2009 lilipoanza kampeni yake ya mashambulizi.

Matangazo

IJUE DW

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com