1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Jeshi la Myanmar latunguwa droni saba kwenye mji mkuu

Josephat Charo
4 Aprili 2024

Vyombo vya usalama vya Myanmar vimezitungua droni saba katika anga la mji mkuu uliojengwa na jeshi wa Naypyidaw hivi leo.

https://p.dw.com/p/4eQim
Jengo la bunge mjini Naypyitaw.
Jengo la bunge mjini Naypyitaw.Picha: Thomas Imo/picture alliance/photothek

Hayo yamesemwa na utawala wa jeshi katika kile kinachoonekana kuwa shambulizi la nadra kufanywa na wapinzani dhidi ya makao makuu ya madaraka ya utawala huo.

Serikali ya umoja wa kitaifa inayowajumuisha wabunge wa zamani waliotimuliwa katika mapinduzi na ambao sasa wanafanya juhudi za kuupindua utawala wa jeshi ilisema imefanya shambulizi hilo dhidi ya jeshi la Myanmar.

Soma zaidi: Guterres "asikitishwa" na mauwaji Myanmar

Taarifa ya utawala wa jeshi imesema droni nne zilizoelekezwa uwanja wa ndege wa Naypyidaw na droni tatu zilizoelekezwa kitongoji cha Zayarthiri cha mji mkuu Yangon zilitunguliwa na kuharibiwa.

Hakuna vifo vyovyote vilitokea wala uharibu wowote uliosababishwa na droni hizo.