1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Jeremy Corbyn

Jeremy Bernard Corbyn ni mwanasiasa wa Uingereza anaeuhdumu kama kiongozi wa chama cha Labour na kiongozi rasmi wa upinzani tangu 2015. Corbyn amekuwa mbunge wa Islington North tangu 1983.

Kiitikadi, Corbyn anajitanabahisha kama Mdemokrati wa Kisoshalisti. Corbyn alichaguliwa kuwa kiongozi wa Labour mnamo 2015. Idadi ya wanachama iliongezeka wakati wa kampeni za uongozi na baada ya kuchaguliwa kwake. Akikielekeza zaidi chama upande wa kushoto, amependekeza kutaifishwa kwa huduma za kijamii, huduma za reli na sera ya uingiliaji mdogo wa kijeshi na kuondolewa kwa makato kwenye huduma za ustawi na umma. Ingawa ni mkosoaji wa Umoja wa Ulaya, aliunga mkono kambi ya kubaki katika kura ya maoni ya 2016 kuhusu kuondoka kwa Uingereza katika umoja huo.

Onesha makala zaidi