1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Je, unakijuwa kinachowanyima usingizi madikteta?

Mohammed Khelef
22 Septemba 2020

DW imezinduwa kampeni maalum kwa jina la "Kuwakosesha Usingizi Madikteta" ambayo imejitolea kwa ajili ya uandishi usioegemea upande wowote duniani

https://p.dw.com/p/3iqBP
Insomnia | Free Speech | Campaign
Picha: DW

Dhamira yetu: Taarifa isiyoegemea upande wowote kwa wenye mawazo huru

Demokrasia inakabiliwa na changamoto na uhuru unashambuliwa kote duniani. Katika nchi ambako wenye nguvu wanadhibiti habari, watu wanalazimika kufanya maamuzi mabaya. Hiyo ndio sababu tumejitwisha majukumu ya kuwapa changamoto watawala wa kiimla kwa kutoa taarifa zisizoegemea upande wowote,na kupigia debe uhuru wa kujieleza na maadili ya kidemokrasia katika nchi zaidi ya 180 kote duniani. Kwa hili, tunahakikisha madikteta hawapati usingizi mnono.

Namna tunavyounga mkono uhuru wa kujieleza
 
DW inajitahidi kuripoti juu ya masuala magumu kuhusu uhuru wa habari kwa kuimurika mizozo, wahanga wa ukiukwaji wa haki za binadamu na mipang ya kuboresha hali ya sasa, wakati huo huo tukiendeleza mjadala juu ya masuala hayo. Kupitia ripoti na mahojiano na wanaharakati, wataalamu, wasanii, wachora katuni na waandishi wa vitabu kutoka pande zote za dunia, mara zote tunatilia maanani masuala yanayochangia uhuru wa kujieleza na uhuru wa kutoa mawazo. Tangu mwaka 2015, DW imekuwa ikiwatuza watu ambao kila siku wanapambana kulinda uhuru wa kujieleza kwa Tuzo ya DW ya Uhuru wa Kuzungumza (DW Freedom of Speech award). Miongoni mwa waliopata tuzo hiyo ni wanablogu na waandishi habari jasiri - watu wanaopambana kwa ajili ya uhuru wa habari. 

DW Freedom of Speech Award 2020 - ACHTUNG SPERRFRIST!
Tuzo ya Uhuru wa Kuzungumza ya DWPicha: DW

Kufikisha ujumbe  

Wakati huu watu wengi zaidi duniani kote wanaweza kuwasiliana kirahisi kuliko ilivyowahi kuwa kabla. Lakini ni rahisi kusahau kuwa zipo sehemu nyingi ambako uhuru wa habari umebanwa na kutoa mawazo ya ukosoaji ni kosa linaloadhibiwa vikali.

Kupiga vita mienendo ya kudhibiti habari ni kanuni ya msingi ya DW, na tunafanya chini juu kuwapa watu habari wanazozihitaji kuweza kuelewa matatizo na masuala yanayoziathiri jamii zao popote walipo. 

Katika nchi nyingi, udhibiti wa serikali wa miundombinu unaweza kuzifanya habari kuchujwa au kuzuiliwa kabisa. Ndiyo maana mara zote DW inatafuta njia za kukwepa udhibiti huo na kufikisha habari kwa watu wa nchi hizo.

Kwa mfano, watu wanaoishi katika nchi zinazozuia upatikanaji wa taarifa huru, wanaweza kupata vipindi vya DW kwa usalama kabisa kwa kutumia teknolojia ya OTF (Open Technolog Fund) ambayo inawawezesha kupata habari hizo bila kufichua utambulisho wao, na pia mradi wa Tor (The Onion Routing). DW imeweka utaratibu wa kutumia tovuti yake ya dw.com kupitia anuani ya mtandao wa Tor. 

Tovuti zinazopatikana kupitia mtandao wa Tor zinatambulika kwa kipashio tamati cha ''.onion.'' Ni lazima kuwa na brauza maalum kama vile Tor iliyofungamanishwa ndani ya Firefox ili kuweza kuzifikia tovuti hizo. Kando ya DW, hadi sasa ni mitandao ya vyombo vichache tu vya habari kama BBC na The New York Times ambayo inapatikana katika anuani ya onion. 

Mnamo muongo uliopita, DW imekuwa ikitumia pia mfumo uitwao Psiphon kuvikwepa vizuizi vya kuchuja habari. Mfumo huo ambao hufanya kazi kwa kutumia mtandao wa msambazaji tofauti na kiunganishi kati ya mtumiaji na chanzo cha mtandaoni.

DW The 77 Percent Moderatorin Elizabeth Shoo (Artikelbild Detailseite Bio)
Asilimia 77, Vijana Mubashara.

Kwa teknolojia hii, watumiaji katika nchi kama China na Iran wamewezeshwa kupata habari zisizopendelea upande wowote kutoka vyanzo vya kuaminika. 


Kwa kujihusisha na teknolojia hii, tumetuma ujumbe: DW haitaacha kamwe kujaribu kukuza mtandao wa bure na kutoa habari huru, za ukweli na zenye ubora na habari kwa watumiaji wa habari hizo kote duniani.  

Maoni tofauti kuchangamsha mjadala 

Mazingira ya habari na ushiriki katika vyombo vya habari vimebadilika sana katika ulimwengu wa Kiarabu kwa miaka michache iliyopita - na sio tu miongoni mwa vijana. Kila kitu kinabadilika. Na wakati watu wakiwa na uwazi zaidi kwa mawasiliano na majadiliano kuliko hapo awali - upatikanaji wa programu za simu za kisasa na mawasiliano ya kutumia simu za mkononi, unaonekana kuhamasisha ari ya watu kutaka kujifungia wasishiriki kwenye mijadala. JaafarTalk inataka kuibadilisha hali hiyo.

JaafarTalk aus dem jordanischen Flüchtlingslager Zatari
Kipindi cha JaafarTalkPicha: DW

Ni kipindi ambacho kinampa kila mtu sauti, hata zile ambazo hazijasikika katika ulimwengu wa Kiarabu, na mada ambazo haziguswi kwenye vituo vyengine. Kipindi hiki kinaruhusu majadiliano juu ya mada teteza kijamii na kisiasa, kwa mwingiliano wa hoja kati ya washiriki, ambao hutoka nchi mbali mbali wakiwakilisha maoni tofauti.

Mwishoni mwa kila kipindi, watazamaji wote; walioko studioni na walioko majumbani, hupata nafasi ya kupiga kura kuhusu mshiriki aliyejieleza kwa ufasaha zaidi. Ni jukwaa murua kwa watu walio na mitazamo tofauti juu ya suala fulani kuchangia maoni na kuanzisha mjadala.

JaafarTalk ni kipindi shirikishi ambacho humurika mseto wa maoni katika ulimwengu unaozungumza lugha ya Kiarabu. Mwongozaji wa kipindi hicho huwaalika wageni wanaowakilisha maoni tofauti katika ukanda huo, kufanya mjadala wenye uchangamfu na kuvumiliana, ukijumuisha utafiti na vigezo vinavyosaidia kutoa sura halisi ya hali ya mambo. Unaweza kufuata kipindi cha JaafarTalk kwenye Instagram, Facebook na YouTube. 

Kuyamurika masuala 

Corona Virus Fake News
Vipi unaweza kuwa na uhakika wa taarifa unayopokea katika zama hizi za habari za uzushi?Picha: imago images/A. Limbach

Je, raia wa Lebanon hujieleza zaidi kupitia mitandao ya kidijitali kuliko wa Ukraine?  #speakup ni kipimo cha mradi wa Chuo cha DW (DW Akademie) kinachokadiria uhusiano kati ya ushiriki wa kidigitali, uhuru wa kujieleza ma upatikanaji wa habari katika nchi zilizochaguliwa kwa kazi za Chuo hicho kuhusu miradi ya maendeleo ya vyombo vya habari, kwa ushirikiano na mashirika ya ndani ya nchi hizo.

Kwa lengo la kutoa mtazamo wa ushiriki wa kidijitali kwa wakati huu katika nchi hizo, na pia kutambua hatari zilizopo, kipimo cha #speakup husaidia mashirika yanayohusika na maendeleo ya vyombo vya habari, asasi zisizo za kiserikali, waandishi wa habari na wadau wengine, kuboresha mfumo wa kidijitali, uhuru wa kujieleza na pia upatikanaji wa habari. 

Kipimo cha Uhuru wa Habari

Je, uhuru wa vyombo vya habari upo katika kiwango gani nchini mwako? Kipimo cha Uhuru wa Habari hutoa mtazamo kuhusu faharasa mbalimbali za uhuru wa vyombo vya habari. Unaweza kurambaza ramani ya dunia ili kupata data juu ya uhuru wa habari katika kila nchi, na maelezo ya ziada juu ya kila faharasa.

Uaminifu katika bahari ya taarifa za kupotosha

Türkei l Youtube-Sperre
Nguvu ya mitandao ya kijamii ni kubwa hata kwa taifa la Uturuki.Picha: Imago/R. Peters

Ugumu wa kazi ya uandishi nchini Uturuki unaongezeka kila uchao. DW imeshirikiana na BBC, France24 na Sauti ya Amerika (VOA) kuanzisha chaneli kwenye mtandao wa YouTube, ambayo huwawezesha wazungumzaji wa Kituruki kupata habari za kuaminika, ambazo zinawasaidia kuwa na maoni huru. Chaneli ya YouTube ya +90, ambayo imepata jina lake kutokana na namba ya Uturuki katika mfumo wa kimataifa wa simu, hutoa habari huru na za kuaminika, ikiheshimu uhuru wa kuzungumza na kujieleza, na pia mchanganyiko wa maoni tofauti kuhusu mada na masuala mbalimbali.

Vidio zilizopendwa sana, baadhi zikiwa zimetafsiriwa kwa lugha ya Kijerumani, zimetazamwa na mamilioni ya watu. +90 huzungumzia masuala ambayo mara nyingine hayapo kabisa katika vyombo vya habari vya Uturuki, kama vile wakimbizi, ushoga na usagaji na haki za wanawake. Kwa kuyachunguza masuala hayo kwa kina,+90 inaweka wizani katika sura ya maisha ya kila siku, katika nchi hiyo inayobadilika haraka.