MigogoroIsrael
Israel yapata mabaki ya mwisho yaliyozuiliwa Gaza
27 Januari 2026
Matangazo
Kulingana na jeshi, mabaki hayo ni ya afisa polisi Rani Gvili aliyekuwa anazuiliwa Gaza kwa zaidi ya siku 840 na yatarejeshwa kwa ajili ya mazishi.
Kupatikana kwa mabaki hayo kunaweza kuchochea kufunguliwa upya kwa Kivuko cha Rafah kati ya Gaza na Misri, ambacho ni lango kuu la kutoka kwenye eneo hilo lililoloharibiwa, kwa kuzingatia ahadi za Israel.
Mabaki ya Gvili yalizuiliwa Gaza tangu alipouawa katika shambulizi la Hamas la Oktoba 27, 2023 kusini mwa Israel, lililochochea vita vya miaka miwili kwenye Ukanda wa Gaza.