1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Israel yafanya opereshi kwenye hospitali ya Al-Shifa Gaza

18 Machi 2024

Wanajeshi wa Israel wamefanya mashambulio kwenye hospitali ya Al-Shifa ambayo ni kubwa kabisa katika Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4dqDX
Mzozo wa Mashariki ya Kati | Hospitali ya Al-Shifa mjini Gaza
Jeshi la Israel limesema askari wake wanafanya operesheni ya uhakika kwenye eneo la hospitali ya Al-Shifa.Picha: Victor R. Caivano/AP Photo/picture alliance

Walioshuhudia wamesema mashambulio hayo yalifanywa na ndege za kijeshi kwenye eneo ambalo tayari limeharibiwa vibaya.

Jeshi la Israel limesema askari wake wanafanya operesheni ya uhakika kwenye eneo la hospitali hiyo na limeeleza kuwa hatua hiyo ya kijeshi inatokana na taarifa za upelelezi zinazoashiria kwamba hospitali hiyo inatumiwa na magaidi wa kundi la Hamas.

Maelfu ya wapalestina walioyakimbia makaazi yao wamekusanyika kwenye eneo hilo ili kutafuta hifadhi.

Mara kwa mara Israel imewalaumu Hamas kwa kupanga na kuongoza mashambulio kutokea kwenye hospitali.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa hospitali 155 katika Ukanda wa gaza zimeharibiwa tangu kuanza vita vya Israel na Hamas.