1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yaendeleza mashambulizi katika Ukanda wa Gaza

8 Juni 2024

Ukanda wa Gaza umeendelea kushambuliwa Jumamosi hii huku waziri wa Israel anayehusika na vita akitishia kujiuzulu.

https://p.dw.com/p/4goc0
Shambulizi la Israel huko Nuseirat Gaza katika shule inayosimamiwa na UNRWA
Shambulizi la Israel huko Nuseirat Gaza katika shule inayosimamiwa na UNRWAPicha: Bashar Taleb/AFP/Getty Images

Serikali ya Israel inakabiliwa na shinikizo kubwa kutokana na mwenendo wake katika operesheni ya kijeshi huko Gaza.

Kwa mujibu wa mashuhuda na ripoti za waandishi wa habari wa shirika la habari la AFP, mashambulizi ya Israel yalihanikiza maeneo tofauti ya Ukanda wa Gaza na kuelekezwa zaidi upande wa katikati mwa  eneo hilo la Palestina.

Mashambulizi hayo yanajiri, licha ya uchunguzi dhidi ya Israel baada ya ndege zake za kivita kufanya shambulizi kwenye shule inayosimamiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia wakimbizi wa KIpalestina UNRWA.

Jeshi la Israel lilikiri kufanya shambulio hilo katika kambi ya wakimbizi ya Nuseirat, likidai kuwa lililenga kambi ya wanamgambo wa Hamas na kuwaua magaidi 17.