Israel yaanza kuvunja majengo ya UNRWA Jerusalem Mashariki
20 Januari 2026
Vyombo hivyo vya habari vya Israel na Palestina vimethibitisha kuanza kwa ubomoaji wa majengo hayo.
Shirika la UNRWA katika ukanda wa Mashariki ya Kati pia limethibitisha kuwa maafisa wa Mamlaka ya Ardhi ya Israel walihusika kwenye operesheni hiyo.
Katika chapisho kwenye mtandao wa kijamii wa X, mkuu wa UNRWA Philippe Lazzarini amelaani hatua hiyo na kuitaja kuwa "kiwango kipya cha ukiukaji wa wazi na wa makusudi wa sheria za kimataifa, ikiwa ni pamoja na haki na kinga za Umoja wa Mataifa, uliofanywa na taifa la Israeli."
Lazzarini amelitaja tukio hilo kama "shambulio ambalo halijawahi kutokea" dhidi ya Umoja wa Mataifa na kuonya kwamba linaweza kutokea kwa shirika lingine lolote.
Ameongeza kuwa hatua hiyo inapaswa kuchukuliwa kama tahadhari.