1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel inapanga kuendeleza mashambuilizi yake dhidi ya Iran

27 Machi 2026

Waziri wa ulinzi wa Israel, Israel Katz ametangaza mipango ya kutanua mashambulizi yake Iran, huku kukiwa na uwezekano kufanyika mazungumzo kati ya Marekani na Tehran.

https://p.dw.com/p/5BHRl
Griechenland Athen 2026 | Israelischer Verteidigungsminister Israel Katz gibt Erklärung nach Treffen ab
Picha: Thanassis Stavrakis/AP Photo/dpa/picture alliance

Kulingana na Ofisi yake, Katz amesema hatua iliyochukuliwa inatokana na makomborayanayoendelea kurushwa Israel kutoka Iran.

"Mimi na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu tumeionya serikali ya kigaidi ya Iran kuacha kuwashambulia kwa makombora raia nchini Israeli. Licha ya onyo hilo bado wameendelea kutushambulia, kwa hivyomashambulizi ya jeshi letu la IDF nchini Iran yataongezeka na kutanuka hadi kufikia maeneo ambayo yanausaidia utawala huu kutengeneza na kutumia silaha dhidi ya raia wa Israeli. Watalipa gharama kubwa kwa uhalifu huu wa kivita."

Mapema hii leo Iran iliishambulia Israel huku kukiwa hakuna taarifa hadi sasa ya majeruhi wowote. Israel na Marekani zilianzisha operesheni kubwa ya kijeshi dhidi yaIran kwa kile ilichosema ni hatua ya kuizuwia nchi hiyo kumiliki silaha za nyuklia.

Katika mashambulizi hayo yalianza Februari 28 Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei aliuwawa pamoja na viongozi wengine wa juu serikalimni.