Janga
Israel imethibitisha kuanza operesheni ya ardhini Lebanon
16 Machi 2026
Matangazo
Msemaji wa jeshi la Israel la IDF Nadav Shoshani, amesema operesheni yao inawalenga wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran wa Hezbollah pamoja na miundombinu yao.
Operesheni hiyo pia inasemekana kuwa sehemu ya mpango mpana wa kuwalinda raia wa Kaskazini mwa Israel.
Jenerali Shoshani hakusema iwapo IDF itataka kudhibiti maeneo mapya huko.
Kundi la Hezbollah lilianzisha mashambulizi dhidi ya Israel Februari 28, kupinga mauaji ya Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei, yaliyotokea kufuatia mashambulizi ya Israel na Marekani dhidi ya Jamhuri hiyo ya kiislamu.