ISLAMABAD:Musharraf na Bhuto huenda wakafikia maridhiano | Habari za Ulimwengu | DW | 05.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ISLAMABAD:Musharraf na Bhuto huenda wakafikia maridhiano

Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan bibi Benazir Bhuto anatazamiwa kukamilisha mapatano juu ya maridhiano baina yake na rais Pervez Musharraf.

Bibi Bhuto amepanga kurejea nchini Pakistan katika wiki mbili zijazo ambapo anatarajiwa kushiriki katika uchaguzi mkuu unaotazamiwa kufanyika mwaka ujao.

Mapatano hayo yatakayo kamilishwa baina yake na rais Musharraf yatamwondolea mwanasiasa huyo mashataka ya rushwa yanayomkabili, aidha ataweza kushiriki katika uongozi pamoja na rais Musharraf.

Bibi Bhuto amekuwa anaishi katika hifadhi ya kisiasa mjini London nchini Uingereza kabla ya jenerali Musharraf atwae madaraka mnamo mwaka 1999.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com