Infantino kugombea bila kupingwa kuwa rais wa FIFA | Michezo | DW | 06.02.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Infantino kugombea bila kupingwa kuwa rais wa FIFA

Rais wa shirikisho la kandanda duniani FIFA Gianni Infantino anatarajiwa kutumikia kipindi cha pili cha uongozi baada ya shirikisho hilo  kusema Jumatano atakuwa mgombea pekee katika uchaguzi utakaofanyika mwezi Juni.

Gianni Infantino (picture-alliance/Sputnik/A. Filippov)

Rais wa FIFA Gianni Infantino

 Infantino  mwenye  umri  wa  miaka  48  amekuwa  akiendesha shirikisho  hilo  la  FIFA  tangu  Februari  mwaka  2016.

wakati  huo  huo rais  wa  shirikisho  la  kandanda  nchini  Ujerumani DFB , Reihard Grindel ametoa  wito  kwa  rais  wa  FIFA Gianni  Infantino  kuweka  mahusiano  na  shirikisho  la kandanda  barani  Ulaya  kuwa  mazuri  muda  mfupi  kabla  ya  kuchaguliwa  tena  katika baraza  la  shirikisho  hilo  la  kandanda  duniani.

Reinhard Grindel (picture-alliance/dpa/B. Thissen)

Rais wa shirikisho la kandanda la Ujerumani DFB , Reinhard Grindel

"Nitakuwa na  furaha  kubwa iwapo  tutakuja  pamoja  katika  ushirikiano wenye  maana  kati ya  FIFA  na  UEFA. Hii  hata  hivyo  inahitaji  uwazi  na tafakuri  katika  maslahi ya  Ulaya kutoka  upande  wa  FIFA,"  Grindel ameliambia  shirika  la  habari  la  dpa kabla  ya mkutano  wa  kamati ya  utendaji  ya  UEFA mjini  Rome siku  ya  Jumatano(06.02.2019).

Grindel anagombea  bila  kupingwa  ili  kuchaguliwa  tena  kuingia  katika  baraza  la  FIFA na hakutoa  ahadi, hata  kama  kulikuwa  na  mzozo  kati  ya  vyombo  hivyo  vya  Ulaya  na dunia  kwa  muda  sasa.