Infantino azungumzia Nyaraka za Panama | Michezo | DW | 12.04.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Infantino azungumzia Nyaraka za Panama

Rais wa FIFA Gianni Infantino ameelezea ripoti za vyombo vya habari kuhusu mkataba wa Televisheni ambao umeibuka katika nyaraka za siri za Panama zilizovuja kuwa zinatia aibu

Infantino, aliyechaguliwa kuwa rais mpya wa shirikisho hilo la vyama vya kandanda duniani mwezi Februari , ameliambia gazeti la Kicker la Ujerumani katika mahojiano yaliyochapishwa leo Jumatatu (11.04.2016) kuwa mkataba huo wa televisheni aliutia saini kama mkurugenzi wa sheria wa shirikisho la kandanda la Ulaya UEFA , ulikuwa juu ya chombo hicho.

Raia huyo wa Uswisi mwenye umri wa miaka 46, katibu mkuu wa zamani wa UEFA , amesema anaukaribisha na hana wasi wasi kabisa na uchunguzi unaofanywa na maafisa wa ofisi ya mwendesha mashitaka ya Uswisi. Ugunduzi katika kile kinachojulikana kama Nyaraka za Panama unaonesha kwamba Infantino alitia saini mkataba huo kuhusu haki za kuonesha michuano ya Champions League katika TV pamoja na kampuni inayomilikiwa na ndugu kutoka Argentina Hugo na Mariano Jinks, ambao wameshitakiwa nchini Marekani mwezi Mei katika uchunguzi wa ulaji rushwa.

Lakini Infantino ameliambia gazeti la Kicker utoaji wa haki hizo za TV ulikuwa sahihi na kuelezwa kwa makini na haki hizo zilipitia katika utaratibu wa tenda.

Viktor Skripnik atabakia kuwa kocha wa Werder Bremen licha ya kuporomoka hadi katika eneo la hatari katika msimamo wa ligi ya Bundesliga , amesema meneja mkuu Thomas Eichin

"Nimetathmini hali na kuangalia Viktor yuko imara kiasi gani. Wote tunahisia kuwa ni imara kwa kiasi cha kutosha," Eichin amesema.

Eichin ameongeza hajafanya mazungumzo na makocha wengine baada ya Bremen kuporomoka katika robo ya mwisho ya eneo la hatari baada ya kufungwa mabao 2-1 na Augsburg nyumbani siku ya Jumamosi.

Mwandishi: Sekione Kitojo / rtre / afpe / dpae / ZR
Mhariri:Iddi Ssessanga