1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Imran Khan na mkewe washtakiwa kwa ufisadi

Amina Mjahid
27 Februari 2024

Mahaka nchini Pakistan imemtia hatiani waziri mkuu wa zamani Imran Khan na mke wake Bushra Bibi kwa tuhuma za kupokea rushwa.

https://p.dw.com/p/4cvRu
Pakistan Karachi| Maandamano ya kupinga udanganyifu katika uchaguzi
Imran Khan amekuwa mwiba mchungu kwa jeshi la Pakistan lenyeushawishi mkubwa.Picha: Rizwan Tabassum/AFP/Getty Images

Chama cha Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan Imran Khan kimesema Mahakama moja nchini humo imemshitaki Khan aliyekorokoroni pamoja na mkewe Bushra Bibi kwa madai ya kupokea kiwanja kama hongo wakati wa uongozi wake. Wote wawili wamekanusha mashitaka hayo.

Khan aliye na miaka 71 amefungwa jela tangu mwezi Agosti kwa madai ya mengine aliyoyakanusha. Tayari alishashitakiwa kwa madai mengine ya ufisasi yaliyompiga marufuku ya kushiriki katika masuala yoyote ya kisiasa Pakistan kwa muda wa miaka 10.

Wagombea wallioungwa mkono na chama cha Khan cha Pakistan Tehreek-e-Insaf (PTI)  katika uchaguzi uliomalizika hivi karibuni walishinda viti vingi bungeni lakini vyama vya upinzani vilivyoongozwa na Nawaz Sharif na Bhutto viliungana pamoja kuunda serikali ya mseto.