1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi ya vifo kufuatia mafuriko Kenya yafikia watu 181

2 Mei 2024

Idadi ya vifo kufuatia mafuriko na maporomoko ya ardhi tangu mwezi Machi nchini Kenya imefikia watu 181, huku mamia ya maelfu ya wengine wakilazimika kuyahama makazi yao.

https://p.dw.com/p/4fQBp
Kenia Nairobi Hochwasser
Maji yakiwa yamezunguuka nyumba katika nchini KenyaPicha: SIMON MAINA/AFP/Getty Images

Eneo la Afrika Mashariki limekumbwa na mvua kubwa zinazohusishwa na mfumo wa hali ya hewa wa El-Nino, na kusababisha mafuriko ambayo tayari yamepelekea vifo vya makumi ya watu katika nchi jirani za Tanzania na Burundi, na kuharibu nyumba za makazi, barabara, madaraja na miundombinu kadhaa.

Ikulu ya White House imetuma salamu za rambirambi kwa familia za waathiriwa na kusema Marekani inachangia katika juhudi za kukabiliana na maafa hayo.

Soma pia:Mafuriko yakwamisha watalii karibu 100 Maasai Mara

Rais wa Kenya William Ruto alitangaza kuwa watu wote wanaoishi katika maeneo yenye hatari ya kukumbwa na mafuriko watahamishiwa maeneo salama.