1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UhalifuUfilipino

ICC kuanza kusikiliza kesi ya awali ya Duterte wa Ufilipino

23 Februari 2026

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu - ICC itaanza kikao cha kuamua kama rais wa zamani wa Ufilipino Rodrigo Duterte anapaswa kushtakiwa kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu unaohusishwa na msako wake dhidi ya dawa za kulevya.

https://p.dw.com/p/59ENi
Rais wa zamani wa Ufilipino Rodrigo Duterte
Duterte, ambaye alikuwa rais kuanzia mwaka 2016 hadi 2022, alikamatwa mjini Manila mwezi Machi mwaka 2025Picha: Aaron Favila/AP Photo/picture alliance

Kikao hicho cha "uthibitisho wa mashtaka", kinachofanyika kwa siku nne, kitaamua kama kuna ushahidi wa kutosha dhidi ya Duterte kuendelea na kesi. Rais huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 80 hatakuwepo katika kikao cha mahakama huko The Hague baada ya mahakama kukubali ombi la utetezi la kuondoa haki yake ya kuhudhuria, licha ya majaji kuamua kwamba alikuwa anafaa kushiriki. Baada ya kusikilizwa kwa kesi hiyo, majaji watakuwa na siku 60 kutoa uamuzi wa maandishi.

Waendesha mashtaka wa ICC wamemshtaki Duterte kwa makosa matatu ya uhalifu dhidi ya binadamu, wakidai kuhusika kwake katika mauaji ya watu wasiopungua 76 kati ya mwaka 2013 na 2018. Idadi halisi ya mauaji wakati wa kampeni yake nchini Ufilipino inadhaniwa kuwa ni maelfu, na mawakili wa waathiriwa wamesema kwamba kesi kamili inaweza kuhamasisha familia nyingi zaidi kujitokeza. Duterte, ambaye alikuwa rais kuanzia mwaka 2016 hadi 2022, alikamatwa mjini Manila mwezi Machi mwaka 2025, akasafirishwa kwa ndege hadi Uholanzi na tangu wakati huo ameshikiliwa katika Gereza la Scheveningen.