HRW: Kenya ichunguze mauaji ya waandamanaji | Matukio ya Afrika | DW | 21.06.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

HRW: Kenya ichunguze mauaji ya waandamanaji

Shirika la kutetea haki za binadamu Human Rights Watch limesema watu watano waliuliwa na wengine 60 kujeruhiwa na polisi katika mandamano ya CORD mkoa wa Nyanza. Otsieno Namwaya wa HRW azungumza na DW.

Sikiliza sauti 03:05

Mahojiano na Otsieno Namwaya wa HRW

Human Rights Watch imetoa ripoti yake ya utafiti inayolituhumu jeshi la polisi nchini Kenya kutumia nguvu ya ziada kuwatawanya waandamanaji katika mkoa wa Nyanza magharibi mwa nchini hiyo mnamo Mei 23 na Juni 6 2016 ambapo watu watano waliuawa na wengine 60 kujeruhiwa. Maandamano hayo yaliitishwa na muungano wa upinzani nchini Kenya, CORD, unaotaka kuvunjwa kwa Tume Huru ya Mipaka na Uchaguzi ya nchi hiyo, IEBC. Isaac Gamba amezungumza na Otsieno Namwaya ambaye ni mtafiti wa shirika hilo kanda ya Afrika kutaka kujua walichobaini katika utafiti huo.

Sauti na Vidio Kuhusu Mada