Havana yakanusha Castro kuwa na kansa | Habari za Ulimwengu | DW | 18.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Havana yakanusha Castro kuwa na kansa

Havana. Maafisa wa serikali ya Cuba wamekanusha uvumi ya kwamba kiongozi wa nchi hiyo Fidel Castro ana ugua Kansa.

Maafisa hao waliuambia ujumbe maalum kutoka Marekani unaotembelea Cuba kuwa, Castro mwenye umri wa miaka 80 atarejea katika shughuli zake za kawaida hivi karibuni.

Castro hajaonekana katika hadharani toka mwezi wa saba mwaka huu alipokabidhi kwa muda madaraka kwa mdogo wakeRaul.

Ujumbe huo wa watu kumi kutoka serikali ya Marekani, ni wa kwanza mkubwa toka mapinduzi ya Castro mwaka 1959. Mjumbe huo uko katika ziara ya siku tatu ukiwa na nia ya kuimarisha uhusiano kati ya Cuba na Marekani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com