Hatma ya Assange kuamuliwa Uingereza | Matukio ya Kisiasa | DW | 24.01.2022
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Hatma ya Assange kuamuliwa Uingereza

Mahakama kuu ya Uingereza inajiandaa kutoa uamuzi  kuhusu ikiwa mwanzilishi wa mtandao wa kufichua siri WikiLeaks Julian Assange anaweza kuyapeleka mapambano yake katika mahakama ya juu zaidi ya Uingereza  

Mapambano ya Julian Assange ni ya kupinga hatua ya Marekani ya kutaka apelekwe nchini humo kushtakiwa.

Uamuzi utakaotolewa wa mahakama kuu ya Uingereza, ni hatua ya karibuni katika mapambano ya muda mrefu wa Assange ya kujaribu kuzuia kupelekwa Marekani kukabiliana na mashtaka ya udukuzi kufuatia kadhia ya kuchapisha nyaraka za siri kupitia mtandao wake wa WikiLeaks, zaidi ya muongo mmoja uliopita.

soma zaidi:

Jaji wa mahakama ya wilaya mjini London alilipinga ombi la Marekani la kudai Assange apelekwe nchini humo, jaji huyo akitumia sababu za msingi kwamba Assange alikuwa na uwekezano wa kujiua ikiwa atashikiliwa chini ya mazingira magumu katika jela ya Marekani.