Hamburg yaikomea Cologne 2:1 | Michezo | DW | 08.12.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Hamburg yaikomea Cologne 2:1

Katika Bundesliga Hoffenheim bado kileleni licha ya kuchapwa 2:1 na B.Munich.

Katika Bundesliga-Ligi ya Ujerumani,Hamburg ilitamba jana kwa mabao 2-1 mbele ya FC Cologne wakati Wiolfsburg imeitimua nje Hannover pia kwa mabao kama hayo.

Liverpool yaongoza kwa pointi 1 Premier League-ligi ya Uingereza na katika La Liga-ligi ya Spain,FC Barcelona imefungua mwanya wa pointi 9 kileleni mbele ya mahasimu wao wakubwa Real Madrid.

Na huko Afrika Mashariki,Taifa Stars-Tanzania inajiwinda kwa changamoto yake mwishoni mwa wiki ijayo na Sudan mjini Khartoum.

Tuanze na Bundesliga ambayo ijumaa iliopita ilijionea changamoto ya kukata na shoka kati ya mabingwa Bayern Munich na chipukizi waliopanda daraja ya kwanza msimu huu-Hoffenheim.

Jana lakini mapambano 2 yalikamilisha kalenda ya Bundesliga mwishoni mwa wiki pale Wolfsburg ilipoitandika Hannover mabao 2-1 na Hamburg wakatamba mjini Cologne pia kwa mabao 2-1.Alikua Mladen petric alietia mabao yote 2 ya Hamburg,kwanza mnamo dakika ya 15 ya mchezo na utamu ulipomkolea akarudi tena mnamo dakika ya 31 kuupiga msumari wapili na wa mwisho katika jeneza la FCCologne, iliotamani ushindi kuzuwia kulazwa kwa mara ya 4 mfululizo.

Nahodha wa FC Cologne, Mslovenia Novakovic akaipatia Cologne bao mnamo dakika ya 83 ya mchezo,lakini halikutosha kuipatia Cologne hata pointi 1.lngawa Cologne imepoteza mechi 4 mfululizo,haiko hatarini kurudi daraja ya pili ,kwani ina kinga ya pointi 7 kutoka eneo la hatari hiyo.

Katika changamoto ya pili ,Hannover ikicheza na wachezaji 10 tu ,ilishindwa kufua dafu mbele ya Wolfsburg ilioitimua Hannover kwa 2-1.Hilo ni pigo jengine kwa hannover inayopepesuka mkiani mwa Bundesliga msimu huu.

Bayer Leverkusen ilirudi kutamba jumamosi ilipoikumta Borussia Moenchengladbach kwa mabao 3-1 na sasa ina pointi 31 wakati Hertha Berlin waliteleza walipozabwa bao 1-0 na Schalke.Mabingwa wa 2007 Stuttgart chini ya kocha mpya Markus Babbel,wameitandika Cottbus.Eintracht Frankfurt ikatamba mara hii ilipoicharaza Bochum mabao 4-0.Bremen lakini iliendelea kupepesuka na imekomewa bao 1-0 na Karlsruhe.Dortmund na Bielefeld zilitoka suluhu bila ya bao.

Kilele cha Buindesliga mwishoni mwa wiki lakini kilianzia ijumaa pale Bayern munich ilipotolewa jasho na chipukizi Hoffenheim.

Ilikua Ivesebic kama kawaida alielifumania kwanza lango la B.Munich ,lakini Philipp Lahm ,beki mshahara wa B.Munich aka