Gianni Infantino kugombea urais wa FIFA | Michezo | DW | 27.10.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Gianni Infantino kugombea urais wa FIFA

Katibu mkuu wa Shirikisho la Kandanda ulaya (UEFA) Muitaliano Gianni Infantino amejitosa kwenye kinyang‘anyiro cha kuwania urais wa Shirikisho la Kandanda Duniani - FIFA.

Infantino, anaungwa na mkuu wa UEFA aliyesimamishwa uongozi kwa muda Mfaransa Michel Platini, kuwania nafasi hiyo ya kuongoza FIFA.

Rais wa Shirikisho la Kandanda la Asia Sheikh Salman bin Ebrahim Al Khalifa pia amethibitisha kuwania wadhifa huo wa kumrithi Mswisi Sepp Blatter.

Wengine wanaowania kiti hicho cha urais wa FIFA ni Mosima Gabriel maarufu kama Tokyo Sexwale, wa Afrika Kusini, Mwanamfalme Ali Bin al-Hussein wa Jordan, David Nakhid, wa Trinidad and Tobago, Jerome Champagne wa Ufaransa, Musa Bility na Segun Odegbami wa Nigeria

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Daniel Gakuba