1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GENEVA: Sudan yakosolewa vikali

9 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD4V

Kamishna wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa, Louise Arbour, ameikosoa vikali serikali ya Sudan akisema inajaribu kubadili wizani wa kikabilia katika jimbo la Darfur.

Katika taarifa yake, Arbour anadai serikali ya mjini Khartoum inatumia wanamgambo wa janjaweed kufanya mashambulio makubwa dhidi ya raia wa kusini mwa Darfrur. Mamia ya raia wameuwawa katika siku nne zilizopita.

Ripoti hiyo iliyoandaliwa kufuatia mahojiano na manusura wa mashambulio yaliyofanywa mwezi Agosti na Septemba mwaka huu, inataka kuundwe tume huru ya Sudan itakayokuwa na kazi ya kuwashtaki na kuwahukumu wakiukaji wa haki za binadamu.

Serikali inatakiwa pia isaidie katika usafirishaji wa misaada ya kiutu na madawa.