Gaza. Wapalestina wauwana katika ghasia. | Habari za Ulimwengu | DW | 07.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Gaza. Wapalestina wauwana katika ghasia.

Wapalestina watatu wameuwawa katika mapigano mjini Gaza baada ya rais wa mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas kutangaza kuwa jeshi la usalama la Hamas ni marufuku kuonekana mjini Gaza na kuwataka wanajeshi wa jeshi hilo kuingizwa katika jeshi rasmi la usalama.

Taarifa ya Abbas ni sehemu ya mpango unaotarajiwa wa mabadiliko miongoni mwa wakuu wa jeshi la usalama wenye lengo la kumaliza ghasia zinazozidi kukua katika mamlaka hiyo ya Wapalestina.

Hamas kimelaani taarifa hiyo ya Abbas , wakimshutumu kwa kutoa ruhusa kwa ajili ya mashambulizi dhidi ya wafuasi wao na kutangaza mipango ya kuliongeza maradufu jeshi hilo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com