GAZA: Wapalestina waliokwama Sinai waanza kurejea nyumbani | Habari za Ulimwengu | DW | 29.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA: Wapalestina waliokwama Sinai waanza kurejea nyumbani

Kundi la kama Wapalestina 100 walionasa nchini Misri limeanza safari ya kurejea nyumbani kwenye Ukanda wa Gaza.Inakadiriwa kuwa kiasi ya Wapalestina 6,000 walikwama katika miji iliyo kaskazini mwa Sinai,tangu kundi la Kiislamu la Hamas kudhibiti Ukanda wa Gaza katikati ya mwezi Juni na mipaka ikajafungwa.

Wapalestina wanaorejea nyumbani,watasafirishwa kwa mabasi na kuvuka mpaka wa Israel,kabla ya kuweza kuingia kaskazini ya Gaza kwa kupitia kituo cha mpakani cha Erez.Wapalestina zaidi,wanatazamiwa kupata ruhusa ya kufanya safari kama hiyo katika siku zinazokuja.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com