1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

G7 kukutana Ufaransa kupunguza mvutano na Marekani

26 Machi 2026

Mawaziri wa mambo ya nje wa G7 wanakutana nje ya Paris kuanzia leo Alhamisi huku mataifa ya Ulaya na washirika wake wakitafuta kupunguza tofauti na Marekani kuhusu vita vya Mashariki ya Kati .

https://p.dw.com/p/5B9VB
G7 mkutano I Liverpool
Mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa G7 uliofanyika Liverpool Uingereza mnamo Desemba 12, 2021Picha: Olivier Douliery/AP/picture alliance

Mkutano huo wa siku mbili wa G7 unaofanyika nje ya mji wa Paris, nchini Ufaransa, unakuja katika wakati ambapo Ikulu ya White House ikisema kuwa Rais Donald Trump yuko tayari kwa mashambulizi makali zaidi ikiwa Iran haitakubali makubaliano ya kumaliza vita vya Marekani na Israel dhidi yake.

Katika safari yake ya kwanza nje ya nchi tangu vita hivyo vilipoanza, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Marco Rubio ataungana na wanadiplomasia wenzake wakuu kutoka Canada, Ujerumani, Italia, Ufaransa, Japan na Uingereza, lakini siku ya pili ya mkutano huo.