1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Ethiopia yataka Eritrea iondoe vikosi kwenye eneo lake

8 Februari 2026

Ethiopia imeiamuru Eritrea iviondoe haraka vikosi vyake inavyodai viko ndani ya himaya yake. Nchi hiyo inaishutumu Eritrea kwa kuiingilia na kushirikiana na makundi ya waasi katika upande wake wa kaskazini magharibi.

https://p.dw.com/p/58J36
Ethiopia imeionya Eritrea isishirikiane na waasi ndani ya mipaka yake
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia Gedion TimothewosPicha: Amanuel Sileshi/AFP/Getty Images

Waziri wa mambo ya nje wa Ethiopia Gedion Timothewos kupitia barua yake ya jana Jumamosi amemuambia mwenzake wa Erithrea kuwa, matukio ya siku kadhaa zilizopita yanaashiria kuwa serikali ya Asmara imechagua njia inayochochea mvutano. Barua hiyo imetaka ushirikiano wowote kati ya Eritrea na waasi usitishwe haraka.

Bado diplomasia inaweza kutumika

Hata hivyo Timothewos amesema bado anaamini kuwa hali ya ghasia na kutokuaminiana inaweza kumalizwa kidiplomasia. Hadi sasa Eritrea haijajibu chochote kuhusu shutuma hizo. Eritrea ilipata uhuru kutoka kwa Ethiopia mwaka 1993. Nchi hizo zilipigana vita vikali vya mpaka vilivyowauwa maelfu ya watu mwaka 1998 hadi 2000.

Nchi hizo zilishirikiana kwa muda, wakati wa mzozo wa Tigray zilipokuwa zikipambana na vikosi vya eneo hilo. Mahusiano yalizorota baada ya Ethiopia kusaini makubaliano ya amani ambayo hayakuihusisha Eritrea mwaka 2022.