1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ethiopia, Somaliland zakubaliana katika matumzi ya bandari

Sudi Mnette
2 Januari 2024

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amesema nchi yake imetia saini mkataba wa makubaliano na eneo lenye mamlaka yake la Somaliland ili iweze kutumia bandari yake ya bahari ya Sham ya Barbeda.

https://p.dw.com/p/4amRT
 Ethiopian airstrike in Finote Selam I Amhara Abiy Ahmed
Picha: AP/picture alliance

Kwa muda mrefu Ethiopia imekua ikiitegemea zaidi nchi jirani ya Djibouti, katika ufanyaji wa biashara zake zinazotegemea bandari.Akizungumza katika hafla ya utiaji saini iliyofanyika mjini Addis Ababa, pamoja na Rais wa Somaliland Muse Bihi Abdi, Waziri Ahmed amesema, jambo hilo kwa sasa tayari limekubaliwa na jirani zao wa Somaliland na hati ya makubaliano imeshasainiwa. Rais Abdi kwa upande amesema, mojawapo ya makubaliano katika mkataba huo ni Ethiopia kuitambua Somaliland kama nchi na taifa huru linalojiongoza.Kwa mujibu wa Mshauri wa Usalama wa Taifa, Abiy Redwan Hussien, makubaliano hayo yamefungua njia kwa kuiruhusu Ethiopia kuendesha shughuli zake za baharini katika eneo hilo, nakuiwezeshakukifikia kituo cha kijeshi kilichokodishwa kwenye bahari ya Sham. Somaliland bado haijatambuliwa kimataifa licha ya kutangaza inajitawala tangu mwaka 1991, Somalia imekua ikiendelea kusema Somaliland ni sehemu ya eneo lake.