1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ethiiopia yamkamata mwandishi wa habari wa Ufaransa

Tatu Karema
26 Februari 2024

Polisi wa Ethiopia wamemkamata mwandishi wa habari Antoine Galindo wa jarida la Africa Intelligence la nchini Ufaransa kwa tuhuma za kula njama ya kuanzisha machafuko katika mji mkuu, Addis Ababa.

https://p.dw.com/p/4ctUt
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed.Picha: United Nations FAO 2024

Mwandishi huyo alikamatwa siku ya Alhamis (Februari 23) na alipofikishwa mahakamani siku ya Jumamosi, hakimu aliyesikiliza kesi yake alikubali kuongeza muda wa kuzuiliwa kwa Galindo hadi Machi 1.

Uongozi wa jarida la Africa Intelligence umelaani kukamatwa kwa mwandishi wao na umetaka aachiliwe mara moja.

Soma zaidi: Rais wa Somalia ailaumu Ethiopia kwa kuzuiwa kushiriki mkutano wa Umoja wa Afrika

Wanaharakati wa haki za binaadamu mara kwa mara wameikosoa Ethiopia kwa kubana uhuru wa vyombo vya habari, hasa katika kuandika taarifa muhimu kuhusu migogoro na hali ya usalama nchini humo.

Kamati ya Kuwalinda Waandishi wa Habari yenye makao yake mjini New York, Marekani, imesema takribani wanahabari wanane wamezuiliwa nchini Ethiopia tangu mwezi Agosti 2023.