1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EAC yakanusha katibu mkuu wake kufutwa kazi

Bruce Amani
11 Machi 2024

Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imekanusha kuwa katibu mkuu wake, Peter Mathuki, anakabiliwa na tuhuma za ubadhirifu wa fedha na kwamba ameondoshwa katika nafasi yake.

https://p.dw.com/p/4dP4M
EAC Peter Mathuki
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Peter Mathuki.Picha: Emmanuel Lubega/DW

Jumuiya hiyo yenye makao yake makuu mjini Arusha kaskazini mwa Tanzania, imeipinga  taarifa hiyo iliyochapishwa na gazeti la The East African ikieleza kuwa si ya kweli.

Soma zaidi: Mivutano inazidi kushuhudiwa katika Jumuiya ya EAC

Taarifa ya EAC ilisema siku ya Jumatatu (Machi 11) kwamba katika kipindi cha miaka mitatu cha uongozi wa katibu mkuu huyo hakukuwahi kuwa na taarifa yeyote mbaya ya fedha kutoka kwa "baraza la mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambalo ndio chombo muhimu cha utendaji kazi katika Jumuiya hiyo."

Soma zaidi: Kenya, EU wakaribia kukamilisha makubaliano ya biashara

Taarifa kutoka Kenya anakotokea Mathuki, zinasema Rais William Ruto amemteua katibu mkuu huyo wa EAC kuwa balozi wa Kenya nchini Urusi na kwamba nafasi yake kwenye Jumuiya hiyo yenye mataifa manane wanachama inachukuliwa na Caroline Mwende.