1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaEthiopia

Duru mpya ya mazungumzo kati ya Ethiopia ya Tigray yaanza

Thelma Mwadzaya7 Novemba 2022

Juhudi za kusaka amani ya Ethiopia zimeingia awamu mpya baada ya wajumbe kukutana kwa mara ya pili. Ajenda ni utekelezaji wa mwafaka wa kusitisha mapigano na kubwaga silaha uliofikiwa wiki iliyopita mjini Pretoria.

https://p.dw.com/p/4JA3G
Masuala yanayojadiliwa ni pamoja na jinsi ya kusimamia utekelezaji wa mkataba wa Pretoria
Masuala yanayojadiliwa ni pamoja na jinsi ya kusimamia utekelezaji wa mkataba wa PretoriaPicha: Siphiwe Sibeko/REUTERS

Kwa mujibu wa ibara ya 6 ya mkataba wa amani wa Pretoria, wawakilishi wa pande zote zinazozozana waliridhia kwa makamanda wa ngazi ya juu kukutana siku tano baada ya kutia saini makubaliano ya amani na kujadili mbinu mujarab za waasi wa TPLF kubwaga silaha. Hayo yanategemea pia hali halisi ya usalama nchini Ethiopia. Kwa upande wake, mjumbe wa amani wa eneo la Maziwa makuu na pembe ya Afrika, Rais mstaafu wa Kenya Uhuru Kenyatta ana imani kuwa pande hizo mbili zinazohasimiana zitasitisha mapigano na vurugu hizo zitazikwa kwenye kaburi la sahau.

Rais mstaafu Uhuru Kenyatta alisisitiza kuwa baada ya mchakato huo kukamilika, wote wataungana kupiga vita uadui unaochochea mirindimo ya risasi utamalizwa ili tujikite kwenye juhudi za kuimarisha hali zetu.Uhuru Kenyatta aliyasema hayo kwenye kituo cha Moran kilichoko mtaani Karen hapa jijini Nairobi wanakokutana wawakilishi wa serikali ya Ethiopia na waasi wa Tigray People Liberation Front, TPLF. Kulingana na makubaliano rasmi, pande zinazohasimiana kimsingi zitasitisha mapigano na kubwaga silaha kwenye eneo la Tigray lililogubikwa na vurugu.Kadhalika watajitahidi kumaliza mzozo huo wa miaka 2 haraka iwezekanavyo. Reda Getachaw ni msemaji wa waasi wa TPLF

Raia zaidi ya laki nane wamepoteza maisha 

Duru mpya ya mazungumzo kati ya Ethiopia ya Tigray yaanza
Duru mpya ya mazungumzo kati ya Ethiopia ya Tigray yaanzaPicha: PHILL MAGAKOE/AFP

Wakati huohuo takwimu za Umoja wa mataifa zinaashiria kuwa zaidi ya raia wa kawaida laki nane huenda wamepoteza maisha yao tangu mwezi wa Novemba mwaka 2020 kwasababu ya ukosefu wa chakula na dawa.Wengine milioni 2 huenda wameachwa bila makaazi au kulazimika kukimbilia taifa jirani la Sudan kusaka hifadhi. Redwan Hussein ni mshauri wa maswala ya usalama katika serikali ya Ethiopia

Kufikia sasa, mjumbe wa Umoja wa Afrika AU, Olusegun Obasanjo aliye pia rais wa zamani wa Nigeria, amewapongeza wawakilishi wa pande zote mbili zinazohasimiana kwa kuridhia kukutana ana kwa ana.

Wapiganaji wa TPLF walishikilia kuwa sharti wasitambuliwe kama magaidi ndipo waweke silaha chini.Serikali ya Ethiopia imeridhia hatua hii iliyopendekezwa tangu mwaka uliopita na Uhuru Kenyatta alipokuwa madarakani.

Mazungumzo kuhusu mzozo huo wa Ethiopia yanaongozwa na wapatanishi 3 wa Umoja wa Afrika na mazungumzo yalianza tarehe 25 mwezi uliopita wa Oktoba mjini Pretoria huko Afrika Kusini.