1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la DRC na M23 walaumiana kukiuka kusitisha vita

3 Desemba 2025

Jana Jumanne, jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda wametupiana lawama za kukiuka makubaliano ya kusitisha mapigano.

https://p.dw.com/p/54f0L
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Kibumba 2022 | Watu wanakimbia mapigano kati ya vikosi vya serikali na waasi wa M23.
Watu wanatembea barabarani karibu na Kibumba, kaskazini mwa Goma, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wakikimbia mapigano kati ya vikosi vya Congo na waasi wa M23 katika jimbo la Kivu Kaskazini, tarehe 24 Mei 2022.Picha: Moses Sawasawa/AP Photo/picture alliance

Lawama hizo zinatolewa ikiwa ni siku mbili kabla ya  Ikulu ya Marekani kuandaa hafla ya kusaini makubaliano ya kumaliza mapigano mashariki mwa nchi hiyo. Pande zote mbili zinaumiana kwa kujaribu kuhujumu makubaliano ya amani kupitia mashambulizi katika jimbo la Kivu Kusini. Jeshi limesema wanajeshi wake walishambuliwa katika maeneo ya Kaziba, Katogota na Lubarika na kundi la waasi la M23 pamoja na washirika wake.Corneille Nangaa, kiongozi wa muungano wa waasi unaojumuisha M23, alisema kwenye ukurasa wakw wa X kwamba vikosi vya Congo, pamoja na jeshi la Burundi na washirika wengine, wameanzisha mashambulizi katika jimbo hilo.Marekani na Qatar zimekuwa zikiongoza mazungumzo yanayolenga kurejesha amani katika amjimbo  ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini, ambako mapigano yamesababisha maelfu ya watu kukimbia makazi yao. Rwanda imekana kuunga mkono kundi la M23, ambalo linadai linapigana kulinda jamii za Watutsi mashariki mwa Congo.