1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Donald Trump kumtaja Barrett mrithi wa Ginsburg

Lilian Mtono
26 Septemba 2020

Rais Donald Trump wa Marekani anatarajia kumtaja Amy Coney Barrett kuwa jaji wa mahakama ya juu zaidi nchini humo ikiwa ni kulingana na vyombo vya habari vya nchini Marekani.

https://p.dw.com/p/3j1vs
Medien: Trump plant mit Barrett als Ginsburg-Nachfolgerin (Rachel Malehorn rachelmalehorn.smugmug.com/AP/dpa/picture-alliance)
Picha: Rachel Malehorn/AP/dpa/picture-alliance

Iwapo atathibitishwa Barrett mhafidhina mwenye misimamo mikali atachukua nafasi ya mliberali nguli, jaji Ruth Bader Ginsburg. Rais Trump anatarajiwa kumtaja Jaji Barrett hii leo.

Trump alisema hapo jana kwamba tayari amekwishafanya maamuzi kuhusu chaguo la mrithi wa jaji Ginsburg akijitapa kwamba "lilikuwa zuri mno" lakini alikataa kuweka wazi ni nani hasa. Ikulu ya White House hata hivyo iliwaashiria wabunge wa Republican na washirika wa nje kwamba atamteua Barrett, hii ikiwa ni kulingana na vyombo mbalimbali vya habari vya Marekani.

Iwapo atathibitishwa, Barrett ambaye kwa sasa ni jaji wa shirikisho katika jimbo la Indiana na anayepigiwa upatu miongoni wa wahafidhina atachukua nafasi ya aliyekuwa jaji wa mahakama hiyo Ruht Bader Ginsburg alifariki dunia Septemba 18.

Soma Zaidi:Jaji wa Mahakama ya Juu Marekani Ruth Ginsburg afariki

USA Präsident Donald Trump Wahlkampf PK
Rais Donald Trump anatarajiwa kumtaja jaji huyo licha ya upinzaniPicha: Tom Brenner/Reuters

Trump aliendelea kusitasita kumuweka wazi mteule wake jana jioni wakati aliporejea kutoka kwenye mkutano wa kampeni. Na alipoulizwa iwapo wabunge wa Marekani waliarifiwa kwamba amemteua Barrett, Trump alitabasamu na kuwajibu, "ndicho wanachowaambia?" Aliongeza kuwa "Mtajua kesho."

"Wote ni wazuri. Anaweza kuwa mmoja kati yao. Atakuwa mmoja ya waliopo kwenye orodha" alisema Trump.

Kinachofnyika sasa ni hatua za mwanzo za mchakato wa kumthibitisha hata kabla ya Trump kumthibitisha baadae leo. Mabadiliko ya majaji wa mahakama hiyo kutoka Ginsburg Mliberali nguli hadi mhafidhina mwenye misimamo mikali huenda kukabadilisha kabisa mwenendo kwenye mahakama hiyo.

Nguvu ya kumzuia haipo.

Kwa Trump hatua hii inampa fursa ya kujiongezea muda katika wakati anapojaribu kuwaimarisha wafuasi wake kabla ya mdahalo unaotarajiwa kufanyika wiki ijayo na mgomea wa urais kutoka chama cha Democrats Joe Biden.

USA: US-Präsidentschaftskandidat Joe Biden in Philadelphia, Pennsylvania
Joe Biden, mgombea urais kupitia chama cha Democrats.Picha: Mark Makela/Reuters

Kwa Wademocrtas, ufichuzi huo wa Barrett utapeleka wasiwasi, katika wakati ambapo chama hicho kikipambania kuirejesha mikononi mwake ikulu ya White House pamoja na baraza la seneti.

Warepublicans katika baraza la seneti wanajiandaa kwa ajili vikao vya kumthibtisha wiki mbili zijazo. Wademocrats pia wanajua fika kwamba hawana uwezo wa kuizuia kura ya bunge kuhusiana na hatua hiyo.

"Nina uhakika atateua mtu mwenye msimamo," Kiongozi wa walio wengi katika baraza la Seneti Mitch McConnel alikiambia kituo cha televisheni cha Fox News cha Marekani, akiangazia uteuzi wa rais Trump. "Watu wa Marekani watafuatilia uteuzi huo na kufanya hitimisho, kama tunavyotarajia kuhitimisha, kwamba kweli anafaa kuthibitishwa kuwa jaji wa mahakama ya juu zaidi ya Marekani."

Lakini kiongozi wa Wademocrats kwenye Seneti Dick Durbin alionekana kutoshangazwa sana na hili. Alinukuliwa akisema wanapambana kuhakikisha hili linafanyika haraka iwezekanavyo. "Wanadhani itamsaidia Donald Trump kuchaguliwa tena."

Uchaguzi wa rais nchini Marekani atakayehudumu katika kipindi cha miaka minne ijayo utafanyika Novemba 3 mwaka huu.

Mashirika: DW