Dhaka. Basi lapinduka na kuuwa 40.
7 Januari 2007Matangazo
Nchini Bangladesh kiasi watu 40 wamefariki wakati basi lililokuwa na abiria zaidi ya 100 lilipopinduka na kushika moto kusini mashariki ya mji mkuu Dhaka.
Basi hilo lilikuwa linasafiri kutoka Dhaka kwenda katika mji wa bandari ya Chittagong likibeba abiria wanaokimbia mji huo mkuu kabla ya kuwekwa vizuwizi vya usafiri , vilivyoitishwa na vyama vya kisiasa vitakavyoanza kazi leo Jumapili.
Polisi wamesema kuwa silinda ya gesi katika basi hilo ililipuka na kusababisha moto huo. Vizuwizi vya usafiri kwa muda wa siku tatu nchi nzima vimeitishwa na vyama vya kisiasa vikisusia uchaguzi wa bunge unaotarajiwa kufanyika Januari 22.