Daraja lavunjika na kuuwa watu 15. | Habari za Ulimwengu | DW | 26.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Daraja lavunjika na kuuwa watu 15.

Kathmandu.

Daraja la wapita kwa miguu kuvuka mto katika eneo la magharibi mwa Nepal limevunjika , na kuuwa kiasi watu 15. Inahofiwa kuwa watu wengi zaidi huenda wameuwawa katika ajali hiyo. Watu walioshuhudia wamesema kuwa daraja hilo lilikuwa na watu wengi wakivuka mto Bheri kuhudhuria sherehe za kidini wakati kamba zinazozuwia daraja hilo zilipokatika kutokana na uzito wa watu.

Watu kadha waliangukia mtoni , mita 30 katika maji ambayo yanabaridi kali. Haifahamiki ni watu wangapi hawajulikani waliko , lakini waokoaji wanasema kuwa dazeni kadha za watu huenda wamekufa. Zaidi ya watu 30 wanaripotiwa kuwa wamejeruhiwa vibaya katika mkasa huo ambao umetokea karibu na kijiji cha Chinchu , kilometa 320 magharibi ya mji mkuu Kathmandu.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com