1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Congo yakanusha kukubali operesheni na jeshi la Uganda

Bruce Amani
30 Novemba 2021

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imekanusha kuwa imekubali kufanya operesheni za pamoja na jeshi la Uganda kuwawinda waasi.

https://p.dw.com/p/43eKD
Milizsoldaten Koalition der bewaffneten Gruppen CPC
Picha: Alexis Huguet/AFP/Getty Images

Congo imesisitiza kuwa nchi hizo mbili zinabadilishana tu taarifa za intelijensia.

Ripoti za kuwepo kwa kampeni hiyo ya pande zote za mpakani, ambazo zilithibitishwa na vyanzo viwili vya kidiplomasia, zimezusha wasiwasi miongoni mwa baadhi ya Wakongo, wanaokumbuka jukumu la Uganda katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyomazilika mwaka wa 2003.

Msemaji wa serikali ya Congo Patrick Muyaya amesema majeshi ya nchi hizo mbili yamekuwa yakibadilishana habari kwa miezi mingi, na kuwa hakuna wanajeshi wa Uganda walioko nchini Congo kwa sasa.

Amesema kile serikali ilisema ni kuwa kutakuwa hatua za pamoja za kupambana na waasi na wala sio operesheni za pamoja.

Waasi hao wanatuhumiwa kufanya mashambulizi ya mabomu ya kujitoa muhanga mjini Kampala.

Jeshi la DR Congo layashambulia makundi yenye silaha Kigoma