1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China yazidi kuyaficha makambi ya mateso ya Xinjiang

Iddi Ssessanga
1 Februari 2019

Takriban wanachama milioni moja wa jamii za wachache wanazuiliwa kambini katika mkoa wa mbali magharibi mwa China, Xinjiang. Beijing inasema kambi hizi zinatoa tu mafunzo, lakini kambi hizo zinazidi kupanuka na kutengwa.

https://p.dw.com/p/3Cacw
China Xinjiang Provinz - Kashgar
Picha: Imago/Xinhua/H. Huhu

Mwanzoni fununu zilisambaa kwamba Wauighur wengi waliotoweka mjini Ying, ulioko kati ya milima kaskazini-magharibi mwa China, walikuwa wanashikiliwa katika shule ya zamani ya Kikomunisti.

Baadhi walishikiliwa huko kwa miezi michache, wengine kwa mwaka mmoja au miwili. Wanaume na wanawake wa kila rika. Ndugu zao wakagundua na waliweza kuwatembelea mara moja kwa mwezi na kuwapigia simu kila wiki.

Wengine walishikiliwa kwenye shule ya sekondari, iliyokarabatiwa kuwahifadhi wafungwa kwenye uwanja wa mpira. Wenye wakasema walikuwa wameenda huko kwa ajili ya kusoma.

"Hawawezi kurudi", alisema mwanaume wa Kiuighur anayeishi umbali mdogo kutoka shuleni hapo. Hakuwa na uhakika ni watu wangapi kutoka jamii yake walitoweka, lakini alisema ni wengi tu.

Kasachstan Muslimische Camps in China
Omir Bekali akionyesha wazazi ambao anaamini wanazuwiwa katika kambi nchini China.Picha: picture-alliance/AP Photo/N. H. Guan

'Vituo vya mafunzo ya amali'

Mkoa wa Xinjiang, wenye ukubwa karibu sawa na Iran, umekuwa mahala pa makambi ya kuwazuwilia watu wa jamii za wachache tangu Vita Kuu vya kwanza vya Dunia,  kulingana na wabunge wa Marekani. Takribani watu milioni moja wamewekwa katika kile ambacho serikali ya China inakiita vituo vya "mafunzo ya amali."

Beijing inasema vituo hivyo vinahitajika kuzuwia harakati za kujitenga, itikadi kali za kidini na ugaidi. Wa Uighur, ambao ni jamii ya wachache wanaozungumza Kiturkic, ndiyo wameathirika pakubwa zaidi, lakini kambi hizo pia zimejazwa na Wakazakh, Wa Uzbek, Wakrgyz, Watarta ba Wa Huis, wanaofahamika kama Waislamu wa China.

Baada ya kukabiliwa na ukosoaji mkubwa, maafisa wa serikali ya mkoa wa Xinjiang mwezi Desemba waliandaa ziara zilizopangiliwa vizuri kwenye kambi hizo kwa wanadiplomasia wa magharibi na baadhi ya mashirika ya habari.

Wauighur walioko kwenye kambi hizo walionyeshwa wakiimba, kucheza na kujitenga na kile walichokitaja kuwa hisia zao za zamani za itikadi kali.

Gavana wa mkoa huo Shohrat Zakir aliliambia shirika la habari la Reuters kuwa ripoti za ukandamizaji ndani ya kambi hizo zilikuwa za uongo. Pia alisema wafungwa hao watakuwa wanapungua siku hadi siku.

Lakini uchunguzi wa ndani pamoja na uchambuzi wa nyaraka za mipango rasmi pamoja na data za satelaiti vinaonyesha kuwa kambi hizo siyo zinapanuliwa, lakini zinazidi kutengwa na kutofikika kabisa.

Kasachstan Muslimische Camps in China
Omir Bekali akionyesha wazazi ambao anaamini wanazuwiwa katika kambi nchini China.Picha: picture-alliance/AP Photo/N. H. Guan

Kambi zaongezeka mara nne

Utafiti wa taasisi ya sera za kimkakati ya Australia unaonyesha eneo jumla la kambi 28 mkoani Xianjiang limeongezeka zaidi ya mara nne tangu 2016.

Kambi kadhaa zilizo karibu na maeneo ya mijini zimefungwa katika kipindi cha mwaka uliopita, na vituo vipya vinajengwa au kupanuliwa katika kaunti ambako uingiaji unadhibitiwa kabisaa. Serikali inasema kambi hizo zinafundisha Lugha ya Mandarin ya China, ujuzi wa kazi na sheria za nchi.

Mfumo wa kambi ni mwendelezo wa sera kandamizi dhidi ya Wauighur ambayo ilizidishwa makali baada ya vurugu za kikabila zilizosababisha vifo vya mamia ya Wauighur  katika mji mkuu wa Xinjiang, Urumqi mwaka 2009, na kufuatiwa na mashambulizi yaliolaumiwa kwa WaUighur kwingineko nchini.

Lakini manusura waliliambia shirika la habari la dpa kuwa wlaipigwa, kuteswa na kunyanyaswa ndani ya kambi hizo. Mtafiti wa taasisi ya utamaduni na thiolojia ya Ulaya yenye makao yake nchini Ujerumani, Adrian Zenz anaonya kuwa kiwewe wanachokipata watu kwenye kambi kitazidisha chuki na uasi dhidi ya serikali na jamii ya wengi ya Han.

Mwandishi: Iddi Ssessanga

Mhariri: Josephat Charo