1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China yamulikwa kwa ukiukaji wa haki za binaadamu

31 Mei 2021

Australia na New Zealand zimeonyesha wasiwasi mkubwa kuhusiana na Hong Kong na hali ya haki za binadamu katika mkoa wa Xinjiang, wakati zikinuia kuifuatilia kwa karibu China ambayo ni mshirika wao mkuu wa kibiashara

https://p.dw.com/p/3uDlT
China Boao Forum Xi Jinping
Picha: Ju Peng/Xinhua via AP/picture alliance

Katika mkutano wa kwanza wa ana kwa ana kati ya viongozi wawili wa nchi hizo Scott Morrison na Jacinda Ardern, Australia na New Zealand zimeonyesha kuwa na msimamo mmoja kuhusiana na China.

Kwa sasa Australia haiko katika maelewano mazuri na China ila New Zealand imeboresha mahusiano yake ya kiuchumi na China. Nchi hizo mbili mwaka huu zimeongeza makubaliano yao ya biashara huria.

Wachambuzi wa kisiasa wanasema mambo haya huenda yakaipelekea New Zealand kutochukua msimamo mkali kwa China kuhusiana na masuala ya haki za binadamu.

Lakini Waziri Mkuu wa New Zealand Ardern amekanusha na kusema Australia na New Zealand zina msimamo mmoja katika masuala ya biashara na haki za binadamu.