China yafanya "mashambulizi ya kutishia" dhidi ya Taiwan
24 Mei 2024Kulingana na kituo cha televisheni kinachomilikiwa na serikali ya China, CCTV, kwenye luteka hizo China iliwapeleka pia washambuliaji waliokuwa wamebeba makombora na kufanya kile kilichoitwa "mashambulizi ya kutishia" katika pwani ya Taiwan kwa ushirikiano na wanajeshi wa majini.
China imesema imeanzisha luteka hizo kumuadhibu rais mpya wa Taiwan, Lai Ching-te, na inajaribu uwezo wake wa "kunyakua madaraka" na kudhibiti maeneo muhimu ya Taiwan.
Soma zaidi: Taiwan 'itatetea maadili ya uhuru na demokrasia"
Luteka hizo zilianza siku tatu tu baada ya Rais Lai wa Taiwan kuapishwa.
China inachukulia Taiwan iliyo na mamlaka yake ya ndani kama himaya yake na inampinga Lai kama anayechochea utengano.
Taiwan imelaani vikali luteka hizo na kuitaka China kuacha uchokozi.