1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chelsea inapambana na Blackburn Rovers

14 Januari 2011

Mabingwa wa msimu uliopita, Chelsea, wanatarajiwa kurudisha mchezo wa hali ya juu katika kulitetea taji hilo dhidi ya Blackburn Rovers uwanjani Stamford Bridge hapo kesho.

https://p.dw.com/p/zxio
Frank Lampard anatarajiwa kurudi uwanjani keshoPicha: AP

Katika Michezo, kwenye mashindano ya kandanda ya ligi ya Uingereza - Premier League, mabingwa wa msimu uliopita, Chelsea, wanatarajiwa kurudisha mchezo wa hali ya juu katika kulitetea taji hilo dhidi ya Blackburn Rovers uwanjani Stamford Bridge hapo kesho.

Chelsea Fußball Champions League
Picha: AP

Kocha wa timu hiyo, Carlo Ancelotti, yupo katika shinikizo kubwa la kuipandisha timu hiyo katika nafasi ya juu ya ligi msimu huu. Baada ya kuadhibika kwa kukosekana baadhi ya wachezaji kutokana na kuumizwa wakati wa mechi za nyuma, timu hiyo inatarajiwa kushirikisha wachezaji waliorudi kambini baada ya kupowa maumivu, akiwemo mchezaji wa kiungo cha kati, Frank Lampard, aliye kuwa nje baada ya kufanyiwa upasuaji wa Hernia.

Licha ya kurudi mchezaji huyo nyota wa Chelsea, timu hiyo bado inawakosa wachezaji wengine wakiwemo, John Obi Mikel,Yuri Zhirkov, Alex na Yossi Benayoun.

Wapinzani wa Chelsea wa hapo kesho, Blackburn Rovers, watapatiliza nafasi hiyo na kujaribu kutimiza azma yao ya kujaribu kuwa katika nafasi sita za kwanza msimu huu.

UEFA Champions League Arsenal gegen Schachtar Donezk
Je Arsenal itatoboa?Picha: AP

Ama kwa upande wa washikilia mizinga, 'The Gunners', Arsenal, wana matumaini makuu ya kurudi katika ushindi dhidi ya wapinzani wake mjini London, WestHam.

Mechi ya hapo kesho inafuata matokeo ya siku ya Jumatano wiki hii katika mkondo wa kwanza wa nusu fainali za kombe la ligi, dhidi ya Ipswich Town ambapo Arsenal ilifungwa bao 1-0.

Bado timu hiyo, hatahivyo, ipo katika nafasi nzuri ya ushindi wa taji la Premier League ijapokuwa wana kibarua kigumu ya kuondoa tofauti ya pointi 4 kati yao na timu ya Manchester United.

Mechi ya kesho inatazamiwa kuwa na msisimko kufuatia kushirikishwa kapteni wa West Ham, Mathew Upson, anayesemekana huenda akarudi timu ya Arsenal. Macho yote leo yapo kwake.

Na katika orodha ya mechi za ligi hii ya Uingereza siku ya Jumapili , Birmingham wanapambana na Aston Villa, baadaye Sunderland itaonana na Newcastle na Liverpool dhidi ya Everton, huku Tottenham ikikabiliana na mashetani wekundu, Manchester United.

Mwandishi:Maryam Abdalla/Afpe
Mhariri:Miraji Othman