Cape Verde na Misri zaitoa kimasomaso Afrika kombe la Dunia
16 Juni 2026
Matangazo
Mechi za Kombe la Dunia 2026 zinaendelea kutimua vumbi katika viwanja mbalimbali. Mchezo uliomalizika muda mfupi kati ya Iran dhidi ya New Zealand umemalizika kwa sare ya 2-2.
Katika michezo iliyochezwa hapo awali Cape Verde iliwashangaza wapenda kandanda duniani kwa kutoka sare ya bila kufungana dhidi ya mabingwa wa Ulaya Uhispania.
Katika mchezo golikipa wa Cape Verde Vozinha amezikonga nyoyo za watu kwa umahiri wake aliponyaka michomo ya Uhispania. Kipa huyo amepata zaidi ya wafuasi milioni nne mtandaoni baada tu ya mchezo huo.
Vigogo wa Afrika Misri nao wametoka sare ya 1-1 dhidi ya Ubelgiji.
Leo ni zamu ya Senegal dhidi ya Ufaransa huku Iraq wakiwa kibaruani na Norway.